Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qubanchi, Imamu wa Sala ya Ijumaa wa Najaf Ashraf, alisema katika hotuba zake za Swala ya Ijumaa zilizotolewa katika Husseiniyya Kubwa ya Fatimiyya mjini Najaf Ashraf: “Leo tunakabiliwa na tukio la kimataifa, nalo ni mazishi ya kiongozi wa mapinduzi makubwa zaidi katika historia ya kisasa na Marjii wa dini ambaye aliweza kuongoza Mapinduzi kwa muda wa miaka 37, na hatimaye akapata shahada pamoja na familia yake.”
Aliongeza: “Leo ndiyo mwanzo wa kumuaga shahidi huyu mtukufu. Hapa taifa la Iran linasisitiza kwamba hatufanyi mazishi ya maiti tu, bali tunahifadhi na kuenzi risala na Mapinduzi, haya si mazishi ya mtu mmoja, bali ni uthibitisho wa uhai, leo tunashuhudia mshikamano wa taifa la Iran kwa upande mmoja, na ushiriki wa mataifa makubwa katika kumuaga kiongozi huyu mkubwa kwa upande mwingine, pamoja na kuona uimara wa kusimama dhidi ya vita ambavyo ubeberu wa kimataifa umeanzisha dhidi ya taifa la Iran.”
Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Najaf Ashraf alisema: “Hapa tunakumbuka maneno ya Aqilat Bani Hashim, Bibi Zaynab (sa), aliyomwambia Yazid aliposema:
«فَوَاللَّهِ مَا فَرَيْتَ إِلَّا جِلْدَكَ»
‘Naapa kwa Mwenyezi Mungu, hukuchana chochote isipokuwa ngozi yako mwenyewe.’
Leo, baada ya kupita siku kadhaa tangu taifa la Iraq limkaribishe Shahidi wa zama hizi na kielelezo cha subira, Imam Sayyid Khamenei – Mwenyezi Mungu autukuze zaidi daraja yake duniani na Akhera – wananchi wa Iraq wamesimama imara. Taifa la Iraq linaiambia Iran: Sisi tuko pamoja nanyi; shahidi wenu ni shahidi wetu, vita vyenu ni vita vyetu, na msiba wenu ni msiba wetu.”
Wito kwa Makabila na Wananchi Wote wa Iraq Kushiriki kwa Wingi katika Hafla ya Kumuaga Shahidi wa Zama
Katika muktadha huo, Hujjatul Islam wal-Muslimin Sayyid Sadruddin Qubanchi aliwataka viongozi wa makabila yenye heshima na wananchi wote waumini wa Iraq kushiriki kwa wingi katika hafla hii adhimu ya kumuaga Shahidi wa zama hizi.
Alisema: “Katika siku hizi za Ashura tunaendeleza kumbukumbu ya Karbala na tunasema:
«کذب الموت فالحسین مخلد کلما اخلد الزمان تجدد»
‘Yamesema urongo Mauti, kwa sababu Hussein ni wa milele; kila wakati unapopita, kumbukumbu yake huzidi kuwa mpya.’”
Tunataka Mashia wa Syria Walindwe
Imamu wa Sala ya Ijumaa wa Najaf Ashraf, akizungumzia masuala ya kikanda, alisema: “Tunataka Mashia wa Syria walindwe, kwani kuna taarifa za kushambuliwa kwao na makundi ya kigaidi yenye misimamo ya kimadhehebu mbele ya macho ya utawala uliopo.”
Aliendelea kusema: “Tunawaambia Mashia wa Ahlul-Bayt (as): Mwenyezi Mungu awe Msaidizi wenu. Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi na Mnusuru wenu dhidi ya hila za maadui.”
Kisha akamalizia kwa dua kwa Imam wa Zama (aj), akisema:
«إلهی عظم البلاء وبرح الخفاء وانكشف الغطاء وضاقت الأرض ومنعت السماء وأنت المستعان وإلیک المشتکی وعلیک المعول فی الشدة والرخاء»
“Ewe Mola wangu! Mtihani umekuwa mkubwa, yaliyokuwa yamefichika yamejitokeza wazi, pazia limeondolewa, ardhi imekuwa nyembamba, na baraka za mbinguni zimezuiliwa. Wewe ndiye wa kuombwa msaada, malalamiko yanaelekezwa kwako pekee, na katika shida na faraja tegemeo letu ni Wewe peke yako.”
Maoni yako